+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
1l9wiebjm5r4l1hffdqpwv58e2

Viwango vya CAF vyaiweka Yanga namba moja Tanzania

Orodha ambayo imetolewa jana na Shirikisho la soka Afrika limeonyesha kuwa Yanga inashika Yanga inashika nafasi ya 331 mbele ya Azam FC iliyo katika nafasi ya 351, wakati klabu nyingine ya Tanzania iliyoingia ni Simba  iliyo katika nafasi ya 356.

Msemaji wa TFF, Afred Lucas ameiambia Goal, kushiriki hatua ya makundi ya michuano ya Afrika ndiko kumekuwa kigezo cha Yanga kushika namba moja na kuzitaka timu za Tanzania ziendelee kujipanga ili kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.

“Tunafurahi kuona timu zetu tatu za Tanzania Yanga, Azam na Simba zikishika nafasi za juu Afrika kwani kuna timu nyingi ukanda wetu hazipo kwenye nafasi hizo,” amesema Lucasi.

Esperance ya Tunisia ndiyo inaongoza katika orodha hiyo ikifuatiwa na Etoile du Sahel, zote za Tunisia na TP Mazembe ya DR Congo.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting