+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
h9t9mnihx2bs1i9wrp6zahaq2

Vita Mpya Ufungaji Ligi Kuu Bara 2016/17

Pazia la ligi kuu Tanzania Bara linatarajiwa kufunguliwa agosti 20, ni msimu unaotarajiwa kuwa mgumu hasa kutokana na maandalizi mazuri kwa baadhi ya klabu Vita ya ufungaji msimu huu unatarajiwa kuwa wa upinzani mkubwa sana sababu kuu ni uwepo wa washambuliaji wapya  ligi kuu na wale wazamani kujiandaa vizuri

Msimu uliomalizika tuzo ya ufungaji bora ilikwenda kwa Mrundi Amis Tambwe baada ya kufunga goli 21, akifuatiwa na Hamis Kiiza goli 19, Donald Ngoma 17 na Jeremiah Juma 16

Je kiatu cha ufungaji bora msimu mpya ligi kuu bara kitaenda kwa mzawa au kitabaki kwa wageni kama msimu uliomalizika? Goal inakuletea washambuliaji 7 wenye nafasi ya kunyakua tuzo ya ufungaji bora kwa msimu wa 2016/2017

Amis Tambwe

Mrundi huyu mwenye uwezo mkubwa wa kufunga magoli kwa stahili ya kichwa anatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa wa namba ndani ya kikosi cha Yanga baada ya ujio wa Obrey Chirwa, huyu ndiye mfungaji bora kwa msimu uliomalizika, anatazamiwa kutetea kiatu chake cha ufungaji bora kwa msimu mpya kama akiendelea kupata nafasi ndani ya timu yake

Laudit Mavugo

Mshambuliaji mpya wa Simba anatarajiwa kutoa upinzani mkubwa kwenye vita ya ufungaji bora kwa msimu mpya Tanzania bara  uwezo wake wa kufunga, nguvu alizo nazo  unatazamiwa kuwa changamoto kubwa sana kwa mabeki wa ligi kuu bara, alishafanikiwa kuwa mfungaji bora ligi kuu Burundi kwa vipindi tofauti tofauti

Donald Ngoma

Msimu uliopita alimaliza na magoli 17 ligi kuu, alifanikiwa kutengeneza uwiano mzuri na Amis Tambwe kwa msimu uliomalizika, anatazamiwa kufunga magoli mengi msimu mpya hasa baada ya kuzoea mikiki-mikiki ya ligi kuu bara

Atupele Green

Huyu ndiye mzawa anaye onekana mwenye nguvu ya kukimbazana na wageni kwenye kiatu cha ufungaji bora, mfungaji bora wa kombe la FA tayari amejiunga na JKT Ruvu akitokea ndanda ya Mtwara, anapewa nafasi kubwa ya kumaliza akiwa mfungaji bora kwa msimu mpya kama akipata ushirikiano mzuri ndani ya timu yake mpya

Jeremiah Juma

Amekuwa na msimu mzuri sana kwa miaka miwili iliyopita, msimu 2015/2016 alifanikiwa kumaliza na magoli 16 na ndiye mzawa pekee aliemaliza na idadi kubwa ya magoli kuliko wote, endapo akiendelea kujituma na kuaminiwa ndani ya timu yake anaweza kumaliza mmoja wa wafungaji bora kwa msimu mpya

Ibrahim Fofana

Mshambuliaji mpya wa Azam kutoka Ivory Coast, ana uzoefu wa kutosha kwenye mashindano makubwa ya Afrika, anapewa nafasi ya kuliziba vizuri pengo la Kipre pale Azam ambaye ametimkia Uarabuni

Ibrahim Ajib

Uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira na kufunga ndio sababu ya wadau wengi kuamini msimu huu mshambuliaji huyu wa Simba anaweza kuwa mmoja wa wafungaji bora ligi kuu bara endapo akitumia nafasi vizuri anazopata uwanjani

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting