+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
2725672

Yanga mabingwa wapya Kombe la Shirikisho

Yanga ndio mabingwa wapya wa Kombe la FA baada ya leo kuifunga Azam FC mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Hilo ni taji la tatu kwa Yanga msimu huu baada ya mwanzoni mwa msimu kushinda Ngao ya Jamii na wiki moja iliyopita ilibeba ubingwa wa Ligi ya Vodacom na leo imechukua Kombe la FA likiwa ni la tatu.

Yanga ambayo imepangwa kundi A katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ilianza taratibu mchezo huo na kuwapa Azam nguvu ya kufanya mashambulizi kadhaa kupitia kwa winga wake Farid Mussa.

Azam iliycheza bila nyota wake muhimu kama Pascal Wawa, Kipre Tchetche, Allan Wanga na Salum Aboubakar 'Sure Boy' ilionekana kuumudu mchezo lakini taratibu walionekana kupoteana baada ya Yanga kutawala eneo la kiungo.

Yanga iliyoingia katika mchezo huo wachezaji wake wakiwa katika ari kubwa ikipata bao la kwanza dakika ya 10, mfungaji akiwa Amissi Tambwe aliyeunganisha kwa kocha krosi ya beki Juma Abduli.

Boa hilo lilionekana kuwachanganya Azam na kuwaacha Yanga wakiutawala mcheZo na kutengeneza nafasi nyingi kupitia kwa kiungo wake Haruna Niyonzoma.

Mshambuliaji Donald Ngoma alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga bao la pili kwa timu yake baada ya pasi nzuri ya Deusi Kaseke lakini alijikuta akijigonga na mpira kuokolewa na mabeki wa Azam.

Kari mchezo ulivyokuwa unaendelea Azam ilionekana kurudi mchezoni na katika dakika ya 28 kiungo wake Himid Mao alipiga shuti kali ambalo lilipanguliwa na kipa Deogratius Munishi na mpira kumkuta Farid Mussa aliyeshindwa kumalizia.

McheZo huo uliendelea kuwa wa ushindani mkubwa kwa timu zote kuahambuliana lakini hadi mapumziko matokeo Yanga walikuwa mbele kwa bao la Tambwe.

Kipindi cha pili Azam waliuanza kwa kumtoa nahodha wake a John Bocco na kumuingiza Mrundi Didier Kavumbagu .

Yanga waliingia kwa kasi katika kipindi hicho cha pili na iliwachukua dakika tatu kufunga bao la pili akiunganisha pasi nzuri ya Simon Msuva aliyemlamba C henga beki Gadiel Michael wa Azam.

Boa hilo lilidumu kwa dakika mbili ambapo dakika ya 51 Kavumbagu aliifungia Azam bao la kwanza akiunganisha kwa kifua pasi ya Ramadhani Singano.

Baada ya kuingia kwa bao hilo Azam walionekana kurudi mchezoni na kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga lakini washambuliaji wa Azam walishindwa kuipangua ngome ya ulinzi ya Yanga.

Kuona hivyo kocha Hans van der Pluijm wa Yanga alimtoa kiungo Haruna Niyonzima na kumuingiza Mbuyu Twite ambaye aliongeza uimara kwenye safu ya ulinzi.

Azam waliendelea kupambana kutafuta bao la kusawazisha lakini dakika ya 81, alijikuta walifungwa bao la tatu kupitia kwa kiungo wake Deusi Kaseke aliyeunganisha vizuri pasi ya Thabani Kamusoko.

Boa hilo lilionekana kuwavunja nguvu Azam na kuwaacha Yanga walionyesha Kannada safi huku wakipiga pasi kwenda mbele na kurudi nyuma.

Kocha wa Azam Dennis Kitambi aliamua kumtoa kiungo Farid Mussa aliyekuwa kwenye majaribio nchini Hispania kwenye Klabu ya Tenerife baada ya kushindwa kumpiga beki bora wa michuano hiyo Juma Abduli na nafasi yake kumuongiza Frank Domayo lakini hadi dakika 90 zona kamilika Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-1.

Hui ni ushindi wa kwanza kwa Yanga mbele ya Azam msimu huu kwani kabla ya mchezo wa leo timu hizo ziliweza kucheza mechi nne zote zikamalizika bila kufungana.

Azam wameambulia nafasi ya pili kama iliyokuwa kwenye Ligi ya Vodacom na itaiwwkilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga ingeweza kubeba Kombe medali na Pesa Tsh.5000,0000.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting