+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
9pgwu9beoe5a19wfxzp4zebfa

Usajili wa Yanga uliokamilika kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu

Kuelekea msimu wa mwaka 2017/2018, klabu ya Yanga imeanza kuyafanyia marekebisho kikosi chake maeneo yenye mapungufu kwa kusajili wachezaji ambao watakuja kuwa na mchango wa moja kwa moja kikosini, ili kuweza kutetea taji lake la Ligi Kuu kwa mara ya nne mfululizo kadhalika na mashindano mengine hasa yale ya kimataifa 

Usajili wa Yanga umelenga zaidi kwenye kuziba nafasi za nyota waliotimkia kikosini kama mlinda mlango Deogratius Munish, Haruna Niyonzima na wengine ambao wapo mbioni kutemwa kutokana na kumalizika kwa mikataba au kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Yanga haitaji marekebisho makubwa kwenye kikosi chao tofauti na vilabu vingeni kwani asilimia kubwa wachezaji wake wamesalia kikosini kwa ajili ya msimu ujao, hasa kwenye idara muhimu za ulinzi na ushambuliaji

Goal inakuletea usajili  wa Yanga uliokamilika kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu na mashindano mengine ya ndani na nje ya nchi

Pius Buswita (Mbao FC)

Klabu ya Yanga iIliwapiku wapinzani wao Simba kwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Mbao FC, Pius Buswita, Yanga imempa mkataba wa miaka miwili mshambuliaji huyo, baada ya kufikia makubaliano ikiwa awali kulikuwa na tetesi ya nyota huyo kujiunga Simba baada ya viongozi wa Mnyamakutamba kuwa wamemsajili mchezaji huyo

Abdallah Haji Shaibu "Ninja" (Jang'ombe)

Mlinzi wa kati wa timu ya Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar, Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2016/17, timu ya Yanga, Yanga wamemalizana na kisiki hicho na anatarajiwa kuwa mbadala wa Vincent Bossou 

Ibrahim Ajibu (Simba)

Ndiyo usajili ghali kwa klabu ya Yaanga kuelekea msimu ujao, zaidi ya milioni hamsini za Kitanzania zimetumika kuipata saini ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Wekundu wa msimbazi

Youthe Rostand (African Lyon)

Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba wa miaka miwili kipa aliyekuwa akiichezea African Lyon, Youthe Rostand ambaye ni raia wa Cameroon aliyefanya vizuri msimu uliopita licha ya klabu yake kushuka daraja.

Rostand anaingia Yanga kusaidiana na Beno Kakolanya huku Ally Mustafa akitajwa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Jangwani na amekuwa akihusishwa kujiunga na Singida United kama ambavyo Dida naye anahusishwa kupata dili Afrika Kusini

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting