
#1Victor Valdes | 2002-2014
Ndiye mlinda mlango aliyefanikiwa sana katika historia ya klabu ya Barcelona, mlinda mlango huyo ni mmoja wa nyota waliounda kikosi cha Catalunya kilichobeba mataji mengi katika kipindi chake

#2Dani Alves | 2008-2016
Alijiunga na Barcelona akitokea klabu ya Sevila kwa dau la paundi milioni 30, tangu ajiunga hapo amekuwa mmoja ya mabeki bora Nou Camp na dunia nzima, alikuwa na msaada mkubwa kwa kutoa mchango mkubwa kwenye magoli kadhalika na ulinzi

#3Ronald Koeman | 1989-1995
Ndiye beki mwenye magoli mengi ndani ya Barcelona, amefanikiwa kufunga magoli 102 katika kipindi chake cha miaka 6 alichodumu na Wacatalunya hao. Koeman ana kumbukwa kwa kufunga goli la ushindi katika fainali ya Europe dhidi ya Sampdoria

#4Carles Puyol | 1999-2014
Ni mmoja wa wachezaji waliofanikiwa katika klabu ya Barcelona, mataji sita ya La liga na matatu ya klabu bingwa, Puyol ana sifika kwa roho yake ngumu ya kupambana na kupigania timu yake kwa muda wote alioitumikia Barca

#5Joan Segarra | 1949-1965
Kapteni wa Barcelona kwa miaka ya 1950, ni mchezaji wa tano ndani ya Barcelona alicheza mechi nyingi, Segarra alijitoa sana katika kuitumikia klabu hiyo katika kipindi chake

#6Johan Neeskens | 1974-79
Kiungo mwenye nguvu na mabavu, alikuwa anaweza kufanya kazi za nguvu kwa dakika 90 bila kuchoka

#7Xavi | 1998-2015
Mmoja wa viungo bora kuwahi kutokea Barcelona na duniani nzima, zao hilo la La masia limeche zaidi ya mechi 700 na kufanikiwa kunyakuwa mataji 25, kiungo huyo alikuwa ndiye moyo wa mfumo wa Tik Taka

#8Johan Cruyff | 1973-1978
Ndiyo nembo ya klabu ya Barcelona mafanikio yote wanayo jivunia Wacatalunya hao asilimia kubwa yamechangiwa na Cruyyff, mshindi huyo wa Ballon d'Or 3 amefanikiwa Barcelona kama mchezaji na kocha pia

#9Ronaldinho | 2003-2008
Mmoja wa wachezaji waliobalikiwa kipaji kikubwa cha kuuchezea mpira vile atakavyo, nyota huyo amefanya makubwa ndani ya Catalunya na ni vigumu jina lake kufutika mapema kwa mashabiki wa soka hasa wale wa Barcelona

#10Andres Iniesta | 2002-
Kiungo bora mchezeshaji katika historia ya Barcelona, amekuwa sehemu muhimu ya kikosi tangu enzi za Pep Guardiola hadi sasa

#11Lionel Messi 2004-
Inasemekana ndiye nyota bora kuliko wote walio wahi pita Barcelona, mshindi huyo wa tuzo tano za Ballon d'Or ndiye mfungaji bora wa muda wote katika historia ya klabu hiyo
