+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
1omrfq45gsg4611eghyan2wf37

Makocha wenye leseni kubwa ila bado ni wasaidizi

Ni wakati sahihi kwa makocha hasa wazawa kujiamini na kuanza kuomba kazi ya ukocha kama walimu wakuu na siyo wasaidizi kama sasa ndani na nje ya nchi.

Kufikia msimu wa 2017/2018 Ligi Kuu Bara makocha watakao ruhususiwa ni wale wenye leseni A ya Caf na leseni B kama wasaidizi hivyo walimu wenye leseni C na kuendelea hawataruhusiwa kuwa kwenye benchi la ufundi.

Lengo la TFF ni kuona soka la nchini likipiga hatua kwenda mbele kwa kufundishwa na walimu wenye elimu kubwa ya mpira na ndio maana wamekuwa wakitoa kozi za leseni A na B kila wakati chini ya mkufunzi Sunday Kayuni.

Goal inakuletea makocha wenye elimu kubwa ya ukocha na wana uwezo wa kufundisha klabu yeyote hapa nchini kama walimu wakuu ila bado ni wasaidizi kwa sasa.

Juma Mwambusi

Mwambusi ambaye leseni B aliipata miaka 4 nyuma ni kocha msaidizi wa bingwa mtetezi Yanga, aliwahi kuwa kocha mkuu wa Mbeya City miaka 2 nyuma na kuifanya kuwa moja ya klabu tishio hapa nchini, ni muda wake sasa kutafuta changamoto nyingine ya kuwa kocha mkuu hapa nchini au nje ya nchi sababu elimu na ujuzi wa ukocha anao mkubwa.

Jackson Mayanja

Kocha wa zamani wa klabu za Kagera na Coastal Union ya Tanga, Mganda huyo ni mwalimu mwenye ujuzi mkubwa wa mpira amekubali kuwa msaidizi wa Joseph Omog ndani ya Wekundu wa Msimbazi, leseni yake ya ukocha inatosha kumfanya kuwa kocha mkuu wa klabu yeyote hapa nchini.

Hemed Morocco

Ndiye kocha msaidizi wa Taifa Stars inayonolewa na Charles Mkwasa, Morocco amewahi kuwa kocha mkuu wa Zanzibar kwa vipindi tofauti toauti kulingana na elimu yake kubwa awezi kosa timu ya daraja lolote hapa nchini na nchi za jirani.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting