5lchha0u3jo11dg40k83hjxl9

Simba yamuuzia MO asilimia 51 ya hisa za klabu

Kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba na Mohamed Dewji imefikia muafaka wa kuiingiza klabu hiyo katika uendeshwaji wa mfumo wa hisa kufuatia kikao cha pande zote mbili kilichofanyika jana Dar es Salaam.

Msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara ameiambia Goal, kikao hicho kimefanyika kwa mafanikio makubwa na kufikia maamuzi hayo ambayo anaamini ndio maamuzi ya wana Simba wengi.

Manara amesema katika kikao cha jana, Dewji aliwaeleza rasmi Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba dhamira yake ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20.

Rais huyo wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) baada ya kuuziwa asilimia 51 ya hisa za Simba kwa Sh. Bilioni 20, ameahidi naye atawawezesha wanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo kupewa hisa bure, ambazo wataamua wenyewe kuuza, au kununua hisa zaidi. 

Anataka kuitoa klabu kwenye Bajeti ya Bilioni 1.2 kwa mwaka hadi Bilioni 5.5 na kwa kuamini mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, ameahidi kusajili vizuri, kuajiri kocha mzuri, ambavyo vyote vinaweza kugharimu Sh. Bilioni 4  na kwamba Bilioni 1.5 itakayobaki, ataiweka katika mradi wa ujenzi wa Uwanja.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting