Goal.com
Live
288342

Nani kafanya usajili bora zaidi katika dirisha dogo la usajili?

Dirisha dogo la usajili lililodumu kwa takribani mwezi mmoja limekwisha pita na klabu zote 16 zimekamilisha usajili wake na wako tayari kwa Ligi Kuu na mashindano mengine

Klabu za Simba, Azam na Yanga ndiyo zilikuwa kinara katika dirisha hili dogo kwa kuendelea kumwaga mamilioni ya pesa katika uhamisho wa wachezaji kutoka sehemu mbali mbali mbali ili kupata ubora wanao uhitaji wao

Ungana mna makala hii Goal inakuletea usajili makini na unaoweza zipa mafanikio klabu za Simba, Azam na Yanga.

Samuel Afful- Azam

Ametokea klabu ya Sekondi Hasaacan ya Ghana straika huyu yupo kwenye timu ya taifa ya Ghana chini ya miaka 23, ni moja wa usajili mzuri ndani ya Azam kwanza ni kijana mwenye umri mdogo hivyo wanaweza kuwa nae kwa muda mrefu pia ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga

Daniel Agyei- Simba

Moja ya sababu iliyopekea Mnyama kupoteza pointi kwenye michezo ya mwisho ni makosa binafsi ya mlinda mlango wa kipindi kile Agban ndiyo yali igharimu klabu, ujio wa Agyei utakuwa na faida ya moja kwa moja ni golikipa mzuri kwenye kujilinda na kuzuia mashambulizi makali alifanya hivyo pindi alipokuja na timu yake ya zamani ya medeama kukipiga na yanga kwenye kombe la shirikisho afrika

Yahaya Mohamed-Azam

Mmoja wa washambuliaji wanalo lijua goli vizuri Mohammed, 28, ambaye ni mshambuliaji mzoefu anayetokea Aduana Stars, alikuwa ni mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu ya Ghana msimu uliopita akifunga mabao 15, pungufu ya mabao mawili na kinara Latif Blessing (Liberty Proffessional) aliyetupia 17.

Justice Zulu-Yanga

kwa muda mrefu wana jangwani wamekuwa wakihaha kupata mtu wa kuziba pengo la kiungo mkabaji, ila dirisha hili wamefanikiwa kuinasa saini ya mtu ambaye ana uzoefu na eneo hilo bila shaka kiungo huyu atakuwa msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo

Pastory Anthony-Simba

Ametokea Stand United na kujiunga na Simba ni usajili ambao utakuwa na msaada kwa klabu hasa kutokana na roho yake ya upambanaji pia atakuwa msaada kwa klabu hasa kwa mechi za mikoani kwenye viwanja vibovu ambapo wachezaji wengi wa nje ushindwa kucheza

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting