b319c8zbkan514i242vnnikeo

Kikosi kinachoanza Taifa Stars leo

Kocha wa Taifa Stars Boniface Mkwasa leo amepanga kumwanzisha kipa wa Azam Aishi Manula, katika mchezo wa Kundi G dhidi ya Chad utakaopigwa Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya.

Mchezo huo ni wakufuzu fainali za Mataifa ya Afrika 2017 na Mkwasa ameiambia Goal, kwa kupitia mtandao wa kijamii kuwa amemwanzisha kipa huyo kutokana na kuwa kwenye kiwango bora siku za karibuni.

“Manula yupo kwenye kiwango bora hivi sasa ameisaidia sana timu yake kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki tofauti na Ally Mustapha ambaye ameanza kucheza hivi karibuni ingawa naye yupo vizuri,”amesema Mkwasa.

Kocha huyo amesema mchezo huo ni muhimu kwao kushinda ili kuweka matumaini ya kufuzu kwa fainali hizo hivyo amepanga kikosi kabambe kuhakikisha wanapata ushindi licha ya kucheza ugenini.

Wachezaji wengi watakao anza leo kwenye kikosi cha kwanza dhidi ya Chad ni Shomary Kapombe, Mwinyi Haji Mngwali Erasto Nyoni na Kevin Yondan.
Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Farid Mussa, Mbwana Samatta na Thomas Uliwengu na Farid Mussa.

Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kufufua matumaini ya kwenda AFCON ya mwakani, baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za kwanza za kundi hilo, ikifungwa 3-0 na Misri mjini Cairo na kulazimishwa sare ya 0-0 na Nigeria Dar es Salaam

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting