+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
280629

Usajili uliokamilika kwa klabu za Yanga, Simba na Azam FC.

Vilabu kadhaa vya ligi kuu tanzania bara pamoja na vile vya ligi daraja la kwanza vimeshaanza kunyakua wachezaji wanaodhani watawasaidia kwenye mwendelezo wa ligi hiyo itakayoanza Desemba 12 baada ya kusimama kupisha kalenda ya FIFA na michuano ya Challenge.

Katika harakati hizo za usajili klabu ya Simba tayari imethibitisha kumrejesha mshambuliaji wa KCB ya Kenya Raphael Kiongera, ambaye ilikuwa ikimmiliki na kumtoa kwa mkopo kwenye timu hiyo baada ya mchezaji huyo kupata majeruhi mwanzoni mwa msimu uliopita.

Mbali na kukamilisha usajili huo bado Simba inaonekana kwenye mawindo ikiwa inataka kuimarisha kikosi chake na sasa imeelekeza mawindo yake kwenye kumnyakua winga Brian Majwega anayefanya mazoezi na timu hiyo baada ya kutolewa kwa mkopo na timu yake inayommiliki ya Azam FC.

Azam; hawa ni vinara wa Ligi ya Vodacom msimu huu hadi sasa na wameweza kusajili mchezaji mmoja pekee ambaye ni kipa mkongwe Ivo Mapunda, aliyetemwa na Simba katika dakika za mwisho wakati ligi inakaribia kuanza.

Yanga wao bado hawajasajili mchezaji yeyote mpya wala hawaja acha mchezaji yeyote hadi sasa ingawa inaongelewa kuwa katika mipango ya kusajili mshambuliaji hatari kutoka Afrika Magharibi.

Timu nyingine ambazo hadi sasa zimekamilisha usajili wake kwenye dirisha dogo la usajili ni Mbeya City ambao wameweza kumsajili beki wa kutegemewa wa Coastal Union Tumba Sued 

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0