+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
y2xywj5benqn16zpgroj7jy1x

Takwimu Zamuondoa Mavugo Simba

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayeichezea klabu ya Simba Laudit Mavugo, huenda akatemwa kwenye kikosi hicho katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili na sababu kubwa inaelezwa ni kushuka kwa kiwango chake.

Taarifa ambayo Goal, imeipata kutoka ndani ya klabu ya Simba ripoti ya kocha Joseph Omog, imeelezea kuhitaji asajiliwe mshambuliaji mmoja na kutema mmoja kati ya waliopo kwenye kikosi hicho ambacho pamoja na kusheheni wachezaji wenye majina makubwa lakini hakifanyi vizuri kama ilivyotarajiwa.

"Mavugo ndiye anayefikiriwa kutemwa kwa sababu yeye ni mchezaji kutoka nje na analipwa mshahara mkubwa, lakini mchango wake kwenye timu ni mdogo sana ukilinganisha na thamani tunayompa, uongozi tulimvumilia msimu wote uliopita lakini bado ameshindwa kubadilika msimu huu," amesema mtoa taarifa hizo.

Taarifa hiyo imekwenda mbali na kudai kuwa hawaoni sababu ya kuendelea kubaki na nyota huyo ambaye ukichanganya mabao yake aliyofunga misimu yote miwili hayafikii hata nusu ya mechi wanazocheza msimu mzima hivyo ni vyema wakampa mkono wa kwa heri ili akatafute sehemu nyingine.

Kwa upande wake Mavugo, amesema taarifa za kuachwa kwenye usajili mdogo hana lakini endapo itatokea yupo tayari kuachana na miamba hao wa Tanzania Bara, lakini anaamini hatokosa timu ya kuchezea kutokana na uwezo aliokuwa nao.

Msimu uliopita Mavugo aliifungia Simba, mabao saba kwenye mechi za Ligi Kuu, na msimu huu katika michezo 11, ambayo Simba wamecheza amefunga mabao mawili pekee kitu ambacho kimewachukiza viongozi wa timu hiyo na kuona mchezaji huyo hastaili kuichezea timu yao.

Endapo mpango huo utatimia Mavugo, ataendeleza kasumba ya wachezaji kutoka Burundi kushindwa kutamba wakiwa na kikosi cha Simba, kwani kabla yake walipita wenzake kadhaa na hawakuweza kukubalika na kujikuta wakisitishiwa mikataba yao na kuondoshwa baadhi yao ni Mwinyi Rajabu, Amissi Tambwe, Gilber Kaze na Pierre Kwizera, Warundi wachache waliocheza na kudumu kwa muda mrefu Simba ni Selemani Ndikumana na Ramadhan Wasso




Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0