+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
lerjphnc8l941gckanfb921ay

Real Madrid Ndiye Mbabe wa Ligi ya Mabingwa 'UEFA' asema Bale

Gareth Bale amesema Ligi ya Mabingwa Ulaya ndio michuano ya Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi huku wakipambana kutinga nusu fainali.

Madrid ndio timu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya michuano hiyo mikubwa Ulaya baada ya kutwaa taji lao la 11 msimu uliopita.

Ushindi wa mikuwaju ya penalti dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid uliwaongezea taji lingnie la Ulaya kwenye hifadhi yao ya mataji.

Madrid wameshatanguliza mguu mmoja nusu fainali kufuatia ushindi wa 2-1 katika mechi ya kwanza ugenini dhidi ya Bayern Munich na nyota huyo raia wa Wales amezungumza juu ya ufalme wa miamba hao kuelekea mechi ya Jumanne.

"Daima michuano hii ndio michuano ya Real Madrid. Klabu imeshinda mara 11, kuliko klabu nyingine yoyote," Bale alikiambia Mega kupitia AS Diario.

"Lengo kuu la klabu hii ni kutwaa ubingwa wa UEFA na kutwaa mataji.

"Tunafanya juhudi sana katika mazoezi ili tuweze kutwaa mataji, na tunatumaini kwamba tutapata mataji mengi zaidi."

Bale aliongeza: "Kutinga fainali Ligi ya Mabingwa tunahitaji kuwa na ari. Ukizingatia fainali ya mwaka huu itapigwa kwenye mji wangu wa nyumbani, Cardiff, ni maalumu kwangu na inanipa ari zaidi. Tunafanya jitihada zote ili kufika fainali."

Madrid wanapambana pia kwa ajili ya taji la La Liga.

Vijana hao wa Zinedine Zidane wameizidi Barcelona pointi tatu kileleni mwa msimamo wa ligi na baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Sporting Gijon Jumamosi, bado wanasubiri mechi ya El Clasico baada ya kumalizana na Bayern.

"Nadhani tupo thabiti. Bado hatujafikia ubora wetu wa juu, lakini tunapambana kwa nguvu kufikia malengo," Aliendelea Bale.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0