+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
1061772

Wafahamu wachezaji raia wa DR Kongo waliochezea klabu za Simba na Yanga

YANGA na Simba ndizo timu kubwa zinazoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi Tanzania na nje ya mipaka yake.

Ukubwa kwa Yanga haupo kwenye wingi wa mashabiki tu bali hata kimafanikio ya uwanjani na utajiri wa kifedha.

Yanga ndiyo inaongoza kuchukua kombe la ubingwa wa Tanzania bara mara 24 na wapinzani wao Simba wapo nafasi ya pili kwa kunyakua kombe hilo mara 18.

Mafanikio na uwezo wa kifedha ziliokuwa nayo Yanga na Simba ndiyo timu zilizoanza kusajiliwa wachezaji kutoka nje ya nchi tangu kuanza kwa mfumo wa soka lakimataifa (Proffesion) 1995 wakati huo timu zinazo shiriki ligi kuu zikiwa 20.

Hapo ndipo klabu hizo zikaanza kuonyesha jeuri yao ya fedha kwa kusaka wachezaji wa kusajili kwenye nchi za jirani za Kenya ,Uganda, Rwanda na hata DR Kongo.

Kongo ndiyo nchi ya kwanza iliyofaidika na mpango huo ikifuatiwa na Uganda ambapo klabu hizo zilitumia asilimia kubwa ya pesa zao kusajili wachezaji kutoka huko.

Wachezaji raia wa DR Kongo ambao walifanikiwa kula pesa za matajiri hao kwaupande wa Yanga ni Banza Tshikala, Shaban Nonda ambaye baadaye alicheza klabu ya Monaco ya Ufaransa,

Wengine waliopata bahati hiyo kwa upande wa Yanga ni Petch Kongo, Delo NtumbaPatrick Katalay, Sadic Kalokola,Laurent Kabanda , Sambitumba Iyela na Deo Moke aliyewahi kuichezea Simba

Kwaupande wa Simba wachezaji waliowahi kuichezea timu hiyo raia wa DR Congo ni Lino Musombo, Mutesa Mafisango na Kanu Mbiyavanga.

Hao ndio wachezaji ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa soka la Tanzania na mafanikio ya timu hizo mbili za Yanga na Simba kukuwa .

Wakati fulani Shirikisho la soka Tanzania TFF, iliviruhusu klabu za Tanzania kusajiliwachezaji 10 kutoka mataifa ya nje na hapo ndipo kufuru ikafanyika kwa timu hizo kusajili wachezaji wengi kutoka taifa hilo ambalo limeonekana kuwa na mafanikio ya kisoka ukifananisha na Tanzania.

Mchezaji kama Laurent Kabanda na Nonda Shabani waliweza kuonyesha kiwango kikubwa na hata kuitangaza Yanga na Tanzania kimataifa kutokana na uwezo waliokua nao

Pia nyota hao baada ya kuondoka Yanga walinunuliwa na timu kubwa zaidi Nonda alikwenda Afrika Kusini na baadaye ndiyo akatua Monaco aliyoichezea kwa mafanikio kabla ya kuwa mfungaji wakutegemewa wa timu hiyo.

Kabanda naye baada ya kuondoka Yanga alirudi kwao Congo na kujiunga na mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe inayoongozwa na tajiri Moise Katumbi na aliifanyia mambo makubwa hadi alipofariki dunia miaka mitatu iliyopita.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0