+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
1144192

Vikosi vitavoanza Simba na Yanga kesho

MTANDAO wa Goal unakuletea vikosi vya Simba na Yanga vinavyo tarajiwa kuanza kwenye pambano la Jumamosi la Ligi ya Vodacom Tanzania litakalopigwa uwanja wa taifa Dar es Salaam na kuchezeshwa na mwamuzi Israel Nkongo, ambapo zaidi ya mashabiki 60,000 wanatarajiwa kushuhudia mpambano huo tukianza na wenyeji Simba.

Kocha Dylan Kerr wa Simba, huenda kikosi chake kikawa na mabadiliko ya sura nne mpya ambazo hazikuanza kwenye mchezo wao wa Jumapili iliyopita wakati walipoifunga Kagera Sugar mabao 3-1 kwenye uwanja huo wa taifa ambapo beki kiungo Jonas Mkude anatarajiwa kurudi uwanjani kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeruhi lakini pia wachezaji Juuko Murshid na nahodha msaidizi Mussa Hassan ‘Mgosi’, wanatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza baada ya kukosekana kwenye mechi iliyopita.

1603662

Simba:
1.Manyika Peter
2.Hassan Ramadhan ‘Kessy’
3.Mohamed Hussein ‘Tshabalala’
4.Hassan Isihaka
5.Juuko Murshid
6.Jonas Mkude
7.Awadhi Juma
8.Said Ndemla
9.Hamisi Kiiza
10.Mussa Hassan ‘Mgosi’
11.Peter Mwalyanzi.

Yanga watakao kuwa ugenini kwenye mchezo huo kikosi chao hakitarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa sana na hiyo ni kutokana na matokeo mazuri waliyoyapata kwenye mechi zao tatu zilizopita bila shaka Kocha Hans van der Pluijm, atataka kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili Deusi Kaseke na Mbuyu Twite, na kuwaanizisha Geofrey Mwashiuya na beki Juma Abduli, anayerejea kwa mara ya kwanza uwanjani msimu huu baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye mechi ya mwisho ya msimu uliopita dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

1906942

Yanga:
1.Ally Mustafa ‘Bartherz’
2.Juma Abduli
3.Haji Mwinyi
4.Nadir Haroub ‘Cannavaro’
5.Kelvin Yondani
6.Thabani Kamusoko
7.Simon Msuva
8.Haruna Niyonzima
9.Amissi Tambwe
10.Donald Ngoma
11.Geofrey Mwashiuya

Timu zote zinafanana kwa kuwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zao tatu za awali na kwasasa miamba hiyo ya soka imejichimbia Visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa mchezo huo.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0