+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
f2ja60h2vrm91ui1bhx74k814

Zilizoshuka na Zilizopanda Daraja Ligi Kuu Bara

Msimu wa ligi kuu bara 2015/2016 umemalizika, huku Yanga wakifanikiwa kutetea taji lake kwa mara 2 mfululizo, nafasi ya pili ikikamatwa na Azam, ya tatu samba na nafasi ya nne imekwenda kwa Tanzania prisons ya mbeya.

Baada takribani miezi 8 ya ligi kuu, hatimaye timu za Tanga zote zimeshuka daraja na huku Toto Afrika ,  Ruvu JKT na Kagera Sugar wakiponea Dakika za mwisho.

Goal inakuletea timu zilizo shuka daraja msimu huu ligi kuu bara, na sababu zilizopelekea kushuka ligi kuu na kwenda kucheza daraja la kwanza kwa msimu ujao.

Coastal Union

Msimu huu haukuwa vizuri kwao kutokana na migogoro ya muda mrefu ndani ya klabu baina ya viongozi licha ya kuwa na wachezaji wazoefu katika ligi kuu wameshindwa kuhimili ligi msimu huu lawama zote wakipewa viongozi ambao ni chanzo cha mabingwa hawa wa zamani kushuka daraja, baadhi ya viongozi wameleta matabaka ndani ya klabu na kupelekea mfadhili wa muda mrefu Bwana Bin Slum kujitoa, matatizo ya wachezaji kugoma kwa kukosa posho na mishahara jambo ambalo limeshusha morali ya wachezaji wanachama.

African Sports

Wanashuka daraja baada ya msimu mmoja tangu wapande daraja kwa msimu 2014/2015. Tangu mwanzo wa ligi African Sports ilionesha ni timu ambayo haikujiandaa kucheza ligi kuu, aina ya wachezaji waliosajili , ukitoa udhamini wa Azam na Vodacom hawana vyanzo vingine vya mapato hivyo kupelekea viongozi kuelemewa na mzigo mkubwa wa kuiandaa timu, posho na usafiri.

Mgambo JKT

Wamemaliza nafasi ya tatu kutoka mwisho, waliambulia alama 28 katika michezo 30, licha ya kuwa timu ya tasisi kubwa nchini, Mgambo JKT waliangushwa na uongozi wao, waliachana na kocha wao bora Bakari  Shime, maandalizi ya timu hayakuwa ya kuridhisha sana.

Msimu wa mwaka 2016/2017 timu 3 zimepanda ligi kuu bara kuungana na zingine 13 kwa msimu ujao

Ruvu Shooting

Timu kutoka Pwani, wamerudi ligi kuu bara baada ya kushuka msimu wa 2014/2015, Ruvu shooting wana uzoefu wa kutosha katika ligi kuu , kocha mzoefu Tom Olaba, wachezaji wenye uzoefu na ligi kuu bara kama Kisiga, hivyo haitakuwa na jipya kwao kuzoea mikiki-mikiki ya ligi kuu, kipindi hiki ni muda sahihi kwa benchi la ufundi pamoja na viongozi kuanza kuandaa timu kwa msimu hujao.

Mbao FC

Timu kutoka Mwanza, wanapata nafasi baada ya Geita Gold na Polisi kushushwa daraja kutokana na upangaji wa matokeo katika mechi za daraja la kwanza. Mbao FC ndiyo mara yao ya kwanza kupanda ligi kuu msimu hujao, viongozi wanahitaji kufanya kazi kubwa sana kama kutafuta wadhamini mapema, pesa za Vodacom na Azam haziwezi kuwa msaada kwao, wanaitaji kuongeza wachezaji wasio pungua wa 4 wenye uzoefu na ligi kuu, wasipo jipanga mapema watakuwa kama watalii, watapanda na kushuka kwa msimu mmoja .

African Lyon

Wamekuwa wakipanda na kushuka kwa vipindi tofauti tofauti, kama ilivyo kwa Ruvu Shooting, African Lyon nao wana uzoefu wa kutosha ligi kuu , natarajiwa msimu mpya watatoa upinzani mkubwa maana tayari wameingia makubaliano na tajiri kutoka uarabuni kuifadhili, viongozi sasa waiachie benchi la ufundi kwenye kufanya usajili kama pesa ya huyo tajiri zitatoka.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0