+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
2006762

Breaking News:Nyoso afungiwa miaka miwili kujihusisha na soka

KAMATI ya uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, imemfungia kwa miaka miwili na faini ya Sh. Milioni 2,Nahodha wa Mbeya City Juma Nyoso kwa kitendo cha kumdhalilisha Nahodha wa Azam FC John Bocco.

Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City ambapo timu yake ilifungwa mabao 2-1, Jumapili kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

2006772

Taarifa hiyo ya Tff, imesema imefikia maamuzi hayo baada ya kupitia na kuridhishwa na video za mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya, kutoka Morogoro ambapo baada ya nahodha huyo kufanya kitendo hicho kulitokea vurugu zilizochangia mchezo kusimama kwa dakika kadhaa kusuluhisha jambo hilo.

Kitendo hicho kimelalamikiwa na watu mbalimbali wakiwemo wachezaji wa zamani na wale wanaoendelea kucheza soka kwa sasa na kuitaka TFF, kutoa adhabu kali zaidi kwa mchezaji huyo ambaye imeonekana amezoea kazi hiyo kwa rekodi zinavyo onyesha huko nyuma.

Kabla ya kumfanyia John Bocco Jumampili, msimu uliopita Nyosso aliweza kumfanyia kitendo kama hicho hicho cha udhalilishaji kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Elias Mguri na kufungiwa kutocheza mechi nane za Ligi ya Vodacom, kama haitoshi katika msimu wa 2009/10 Nyosso alimfanyia kitendo hicho beki wa Yanga Amir Maftah na beki huyo kurusnga ngumi ilimsababishia aonyeshwe kadi nyekundu Simba ikishinda kwa mabao 4-3, na msimu wa 2006, Nyosso alimfanyia hivyo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Joseph Kaniki.

Kanuni ya 37 Kifungu cha 24 cha Kanuni za Ligi za TFF toleo la 2015 kinasema: Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi au ya kidhalilishaji au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinaadamu atatozwa faini kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu au/na kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka kumi ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine rasmi ya TFF au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0