+18 | Play Responsibly | T&C's Apply | Commercial Content | Publishing Principles
a7xqkq7d9td91oa5pv76e9ecq

Yanga wanasemaje kuhusu kumsajili Emanuel Adebayor?

Mabingwa watetezi wa ligi ya Vodacom Tanzania Yanga mapema wiki hii walitajwa kuwa katika mipango ya kuinasa saini ya mshambuliaji wakimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor ambaye kwa sasa ni mchezaji huru.

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga inayotajwa kutaka kumsajili nahodha huyo wa taifa la Togo, Baraka Desidedit, ameiambia Goal, kuwa hawajatuma maombi ya kutaka kumsajili mchezaji huyo licha ya kwenye timu ya taifa ya Togo kuwa na mwakilishi wao ambaye ni Vicent Bossou nahodha msaidizi.

“Taarifa hizo hazina ukweli, kwasababu hatumjui wakala wa Adebayor na tunatambua mchezaji huyo malengo yake ni kucheza mataifa ya Ulaya na ASIA na siyo Afrika na sisi kama uongozi tumezipuuza ingawa zimeifanya klabu yeti kujulikana Afrika na hata Ulaya  kutokana na kuhusishwa na usajili wa nyota huyo,”amesema Baraka.

Kiongozi huyo amesema kingine kinachowafanya washindwe kumleta nyota huyo ni kukamilisha idadi ya wachezaji wakigeni ambayo ni saba na pia muda wa usajili ulishapita hadi majira ya kiangazi wakati msimu wa ligi utakapo malizika.

Baraka amekiri kuwa Adebayor ni mchezaji mkubwa duniani na wangefurahi kama wangempata kutokana na ushiriki wao wa michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kanuni zinawabana na wanalazimika kuzisoma habari hizo kwenye mitandao na kuachana nazo.

Adebayor aliyeshindwa kuipa mafanikio timu yake ya Togo kwenye fainali za AFCON zinazoendelea nchini Gaboni, na kujikuta ikitolewa hatua ya makundi ametamba na timu mbalimbali barani Ulaya kama Monaco, Arsenal, Tottenham Hotspurs, Real Madrid na hivi karibuni alikuwa akiichezea  Crystal Palace.

Tetesi za Adebayor kusajiliwa na Yanga zilipokelewaje Tanzania?

Beki wakimataifa wa Togo, Vicent Bossou, ametajwa kuhusika kumshawishi nahodha wake kwenye kikosi cha timu ya taifa hilo Emmanuel Adebayor kujiunga na klabu ya Yanga inayoshiriki ligi ya Vodacom Tanzania ambayo pia ndiyo anayoichezea yeye.

Taarifa zinasema mara baada ya timu ya taifa ya Togo kutolewa mapema katika hatua ya makundi ya michuano ya AFCON, Adebayor alimfata msaidizi wake katika cheo cha unahodha ambaye ni Bossou, na kumwambia kuwa hana timu hivyo amsaidie kutafuta kibarua ndiyo mchezaji huyo akamshauri kutua Yanga ili kuongeza ukali katika ushambuliaji.

Tetesi hizo kabla ya kukanushwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Desidedit zilizua hofu kwa baadhi ya timu zenye upinazani mkubwa na Yanga ambazo ni Simba na Azam akihofia namna gani wanaweza kujipanga ili nyota huyo asiweze kuwadhuru.

Ilikuwa ni faraja kubwa kwa mashabiki wa Yanga ambao siku zote wamekuwa wakipenda kuiona timu yao ikifanya vizuri kila siku ikiwemo kuzifunga Simba na Azam na kuendelea kubeba taji la Ligi ya Vodacom inayolishikilia mara nyingi kuliko timu zote 16 zinazoshiriki ligi hiyo.

Pamoja na uwepo wa Mzimbabwe Donald Ngoma na Amissi Tambwe raia wa Burundi, lakini wanaamini kama Adebayor anatua kwenye timu yao hawataweza kubabaishwa tena na tumu hizo zenye upinzani wa hali ya juu na kikosi cha Yanga ambacho kwasasa kinashika nafasi ya pili kwenye ligi hiyo kwa tofauti ya pointi mbili. 

Yanga ingekuchukuliwaje kama ingefanikiwa kuipata saini ya Adebayor?

Niwazi kama Adebayor angefanikiwa kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga, basi miamba hiyo ya ligi ya Vodacom Tanzania ingechukuliwa kama ni moja ya timu yenyeuwezo mkubwa wa kifedha Afrika Mashariki na Kati.

Yanga ingekuwa timu inayoheshimika na kuogopeka Afrika kutokana na kuwa na mchezaji mwenye jina kubwa Duniani, kutokana na timu alizowahi kuzichezea na rekodi alizojiwekea kipindi akicheza Ulaya.

Hilo linatokana na licha ya kwamba Adebayo kuwa mchezaji huru, lakini klabu hiyo ingetumia kiasi kikubwa cha pesa ili kumsajili na kumpa mshahara mkubwa pengine kuliko mchezaji mwingine yeyote kwenye ligi ya Tanzania.

Licha ya timu za Simba na Azam kutiwa hofu na taarifa hizo lakini hata CAF, nayo ingelazimika kuipangia Yanga timu ngumu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kuwa na nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga wakati akicheza Ulaya.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0