+18 | Play Responsibly | T&C's Apply | Commercial Content | Publishing Principles
179079

Wachezaji bora wa Tanzania wanaocheza nje

GOAL imekuwa makini kufuatilia maendelea ya ukuaji wa soka la Tanzania ikiwemo ufuatiliaji wa wachezaji wake wanaocheza ndani na nje ya mipaka yake.

Hapa Goal inakuletea wachezaji bora wa Tanzania ambao wanafanya vizuri wakiwa huko.

1.Mbwana Samata

Huyu ni mshambuliaji wa klabu bingwa Afrika TP Mazembe ambaye amekuwa na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2011 akitokea Simba ya Tanzania.

Akiwa TP Mazembe msimu wa pili aliweze kuibuka mfungaji bora katika ligi ya DR Congo kwa kufunga jumla ya mabao 13 na kuwapita wakongwe wengi ambao wanatoka nchi mbalimbali zilizo endelea kisoka kama Zambia,Mali na Congo kwenyewe.

Akiwa na TP Mazembe Samata ameweza kushiriki fainali mbalimbali kubwa za Afrika ikiwemo ile ya kombe la Shirikisho CAF, Desemba 2013 dhidi ya CS Sfaxien, na timu hiyo kukamata nafasi ya pili lakini pia mwaka huu aliisaidia timu hiyo kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa na Es Setif ya Algeria.

2.Mwinyi Kazimoto

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka katika klabu ya Al Markhiya, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Qatar.

Kiungo huyu amekuwa na mchango mkubwa katika timu hiyo kiasi cha kufanya timu nyingine kutoka ndani na nje ya taifa hili kumtamani na kutaka kumsajili mchezaji huyo.

Kazimoto ni mmoja ya wachezaji wachache wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa kutoka Tanzania ambaye pia amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’

3.Thomas Ulimwengu

Thomas Ulimwengu huyu ni Mtanzania mwingine anaye cheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya DR Congo

Ingawa Ulimwengu amekuwa akitokea benchi lakini mchango wake kwa timu hiyo ni mkubwa kiasi cha kuchezwa katika kila mechi ambayo mabingwa hao mara mbili wa Afrika wanashuka dimbani.

Ulimwengu tofauti na Samata huenda akazidi kuwa na muda mrefu kukipi katika klabu hiyo kutokana na umri wake kuwa mdogo lakini mchango wake umekuwa ukiwavutia viongozi wa timu hiyo akiwemo mmiliki wake Bilionea Moise Katumbi.

4.Juma Luizio

Mshambuliaji chipukizi wa Tanzania anayecheza soka la kimataifa katika klabu ya Zesco United ya Zambia akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Juma amekuwa ni mchezaji wa kutumainiwa katika kikosi cha Zesco licha ya kuwa na muda mfupi tangu ajiunge na timu hiyo lakini ameweza kuwasaidia mabingwa hao wa zamani wa Zambia kushika nafasi za juu kwenye ligi yao.

Mchango Luizio kwa Zeszo umemfanya mchezaji huyo kuitwa mara kwa mara kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa ajili ya kushiriki mechi mbalimbali za kirafiki na mashindano.

5.Adam Nditi

Nditi ni Mtanzani anayekipa katika klabu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Chalsea ya Uingereza .

Nditi amekuwa na timu hiyo kwa muda wa miaka mitatu sasa lakini tangu afanikiwe kwenda huko hajawahi kuitwa kuzichezea timu za Taifa kwa sababu mbalimbali ikiwemo vibali vyake vya kufanyia kazi nchini.

Utata wa kutokuitwa kwakwe kwenye kikosi cha timu ya taifa unatokana na mchezaji huyo kuondoka Tanzania kwa muda mrefu pasipo mawasiliano ya Shirikisho la soka Tanzania TFF, hivyo mchezaji huyo pamoja na kujulikana kuwa ni raia wa Tanzania lakini bado mpango wa kuitwa umekuwa mgumu.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0