+18 | Play Responsibly | T&C's Apply | Commercial Content | Publishing Principles
112df1z9vgamx1p9udfi200uzd

Usajili ghali zaidi Ligi Kuu Bara

Goal inakuletea usajili wa gharama Ligi Kuu Bara msimu 2016/2017

Obrey Chirwa

Licha ya kutoanza vizuri kwenye klabu ya Yanga kwa kucheza takribani mechi 5 na kutopata hata goli moja, ila Mzimbabwe huyo  ameigharimu Wanajangwani  million 200 kuipata saini yake kutoka Fc Platinums ya Zimbabwe ndio usajili wa pesa nyingi kwa msimu mpya Ligi Kuu Bara.

Laudit Mavugo

Amesaini Simba kwa zaidi ya milioni 100 akitokea Vitalo ya Burundi, takribani miaka mitatu amekuwa akiusishwa kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi bila mafanikio chanzo kikubwa kikuwa ni pesa ila msimu huu amefanikiwa kujiunga na Simba kwa donge hilo nono.

Enock Atta Agyei

Ili mchukua mechi mbili tu dhidi ya Yanga kuonekana na mabosi wa Azam, uwezo mkubwa wa kujilinda na kutawala eneo la kati kuliwavutia wana rambaramba kutoa zaidi ya milioni 60 za Kitanzania kuweza kuvunja mkataba wake kutoka Medeama ya Ghana.
Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0