+18 | Play Responsibly | T&C's Apply | Commercial Content | Publishing Principles
14q77zw4n24bd1t0ixjvaz7ezh

Lionel Messi: Rekodi 5 za dunia anazoshikilia supastaa huyo wa Barcelona

#1 Mshindi wa tuzo nyingi za Ballon d’Or (5)

Ingawa Ronaldo amepunguza pengo dhidi ya Messi miaka kadhaa iliyopita, maestro huyo wa Barcelona bado ametwaa tuzo nyingi binafsi. Mwargentina huyo ametwaa tuzo tano za Ballon d'Or kuliko Ronaldo mwenye tatu.

#2 Mchezaji pekee katika historia kufunga magoli 40+ katika misimu saba mfululizo

Lionel Messi amekuwa thabiti kwa miaka 10 iliyopita tangu msimu wa 2009/2010, legendari huyo wa Argentina alifunga mabao 40+ kila msimu hadi leo.

Barcelona imekuwa klabu yenye mafanikio katika kipindi hiki na magoli ya Lionel Messi ndiyo chachu kubwa ya mafanikio.

#3 Mfungaji wa mabao mengi kwenye Kombe la Dunia la Klabu (5 – sawa na Luis Suarez na Delgado)

Maestro huyo wa Argentina ametwaa ametwaa vikombe vitatu vya Kombe la Dunia la FIFA na haishangazi kuwa amefunga mabao matano. Hata hivyo anashiriki rekodi hiyo na Luis Suarez na Mwargentina Cesar Delgado anayeicezea klabu ya Mexico Monterrey.

#4 Rekodi ya Maajabu ya Dunia kwa idadi kubwa ya magoli yaliyofungwa katika Kalenda (magoli 91 mwaka 2012)

Rekodi za maajabu ya Dunia zinatambua kuwa supastaa wa Barcelona Lionel Messi kuweka historia kwenye kalenda ya mabao 91 mwaka 2012. Mkali huyo wa Barca, 29, alivunja rekodi ya nyota wa Bayern Munich Gerd Muller.

#5 Magoli mengi ya kimataifa katika kalenda ya mwaka  - Klabu na taifa lake (25 mnamo 2012) 

Pamoja na kuingia kwenye kitabu cha historia ya dunia cha Guiness, Messi aliweka rekodi nyingine ya kuwa na magoli mengi ya kimataifa aliyofunga kwenye mwaka mmoja wa kalenda.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0