+18 | Play Responsibly | T&C's Apply | Commercial Content | Publishing Principles
1g9qhffpehwi71koig8162able

Kipa Bora Ligi Kuu ya Vodacom Bara huyu hapa

Kipa wa Azam FC, Aishi Manula, ametajwa kuwa ndiye kipa bora katika Ligi Kuu Bara msimu huu mpaka sasa akiwapiku makipa Deogratius Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Juma Kaseja wa Mbeya City.

Goal kinatambua mchango wa Aishi Manula katika kikosi chake cha Azam FC, hali kadhalika amekuwa akionyesha jitihada katika timu ya Taifa ya Tanzania lakini bado hajafanikiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Charles Mkwasa.

Kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wa zamani wa makipa wa Simba, Mkenya, Iddi Salim, kwa kipindi cha miezi sita alichokaa Tanzania kufundisha soka, amemuona Manula kuwa ndiye bora huku akisisitiza kama ataendelea kulelewa kwenye misingi bora, bila shaka atakuja kuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari Iddi Salim alisema “Kwa miezi sita niliyokaa Tanzania, naweza kusema nimewaona makipa wengi katika Ligi Kuu Bara, lakini kipa wa Azam, Manula, kwangu ndiye ni bora zaidi kuliko mwingine kutokana na mambo anayoyafanya uwanjani ikiwemo kucheza penalti nyingi.

“Lakini pia ukiangalia kwa makipa vijana, Manula anashika namba moja akifuatiwa na Manyika Jr., na kama watazidi kukomaa basi watakuja kuwa makipa wazuri siku za usoni,” alisema kocha huyo aliyewahi kuinoa Gor Mahia na timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars'.

Akizungumzia kipa mwingine bora, Idd alisema Peter Manyika wa Simba, kama atapata matunzo mazuri, mafunzo mazuri na kuthaminiwa, ndiye atakuwa tegemeo la Tanzania hapo baadaye.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0