+18 | Play Responsibly | T&C's Apply | Commercial Content | Publishing Principles
16nfu3zsqu7ri1vpcj27w9ueje

Yanga yacharuka dharau za Haruna Niyonzima

Yanga imecharuka kuhusiana na Haruna Niyonzima kuonyesha dharau kwa uongozi na wanachama wa klabu hiyo Goal imegundua.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alikaririwa na Saleh Jembe amesema wamekuwa hawafurahishwi kwa muda mrefu sasa kutokana na tabia za Niyonzima za kuchelewa kujiunga na kikosi kila anapokwenda Rwanda.

“Niyonzima amekuwa na tabia ambayo si nzuri kwa maana ya nidhamu kila anapokuwa kwao Rwanda. Mfano tumemruhusu kwenda kuitumikia Rwanda katika michuano ya kimataifa, hadi sasa hajarejea.

“Angalia mchezaji wa Azam FC kama Mugiraneza ambaye anacheza timu moja na Haruna amesharejea, wachezaji wa Simba waliocheza fainali wako katika klabu yao.

“Niyonzima hajarejea na wala hasemi lolote. Si Jambo sahihi na hili linaonyesha tabia isiyo sahihi kwa maana ya kuheshimu majukumu yake katika klabu,” alisema Dk Tiboroha.

“Haruna amekuwa akifanya hivi mara kwa mara, lakini sasa tumechoka na kama tutachukua hatua kali, basi wanachama wajue kabisa mapema.

“Tumekuwa tukitoa adhabu kwake mara kadhaa, lakini mambo hayabadiliki. Wakati mwingine tumemkata mshahara hadi sasa tunaona kama tumechoka, lakini mambo ni yaleyale.”

Swali kutoka kwa mhariri: Mashabiki wa Yanga mnasemaje katika swala hili?

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0