Goal inakuletea usajili wa gharama Ligi Kuu Bara msimu 2016/2017
Obrey Chirwa
Licha ya kutoanza vizuri kwenye klabu ya Yanga kwa kucheza takribani mechi 5 na kutopata hata goli moja, ila Mzimbabwe huyo ameigharimu Wanajangwani million 200 kuipata saini yake kutoka Fc Platinums ya Zimbabwe ndio usajili wa pesa nyingi kwa msimu mpya Ligi Kuu Bara.
Laudit Mavugo
Amesaini Simba kwa zaidi ya milioni 100 akitokea Vitalo ya Burundi, takribani miaka mitatu amekuwa akiusishwa kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi bila mafanikio chanzo kikubwa kikuwa ni pesa ila msimu huu amefanikiwa kujiunga na Simba kwa donge hilo nono.
Enock Atta Agyei
Ili mchukua mechi mbili tu dhidi ya Yanga kuonekana na mabosi wa Azam, uwezo mkubwa wa kujilinda na kutawala eneo la kati kuliwavutia wana rambaramba kutoa zaidi ya milioni 60 za Kitanzania kuweza kuvunja mkataba wake kutoka Medeama ya Ghana.