Haruna NiyonzimaGoal Tanzania

Niyonzima: "Yanga haikuwa na Bahati dhidi ya Simba"

Nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima, amesema kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba jana kulitokana na kukosa bahati baada ya kuutawala mchezo kwa asilimia nyingi.

Niyonzima ameiambia Goal, walicheza vizuri na kuwabana wapinzani wao Simba lakini tatizo kubwa kwao ni kushindwa kuzitumia nafasi walizozipata.

“Tumepoteza kwa bahati mbaya na unajua penati hazina mwenyewe, hakuna wakumlaumu zaidi ya kurudi nyumbani ili kujipanga na michuano ya mwakani,” amesema Niyonzima.

Article continues below

Kiungo huyo ambaye jana aliendelea kung'ara kwenye michuano hiyo amesema wanakubali matokeo, hayo lakini wanakwenda kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri sana wenye ligi.

Amesema waliingia kwenye mchezo huo wakiamini wanapata ushindi, lakini mambo hayakuwa kama walivyotarajia ndiyo maana akasema wanayakubali matokeo ya mchezo huo.

“Tunawapongeza Simba, kwa ushindi lakini niwaambie wana Yanga wasife moyo sisi bado tutaendelea kupambana kuhakikisha tunawapa raha kwenye mechi za ligi ambayo itaendelea wiki ijayo,”amesema Niyonzima.

Mchezaji huyo amewataka mashabiki wa Yanga kusahau matokeo ya michuano ya Mapinduzi na kuwapa sapoti kwenye  mechi za ligi ya Vodacom, ili kuhakikisha wanatetea ubingwa wao msimu huu.

“Michuano hii nikama hatuna bahati nayo mwaka jana tulitolewa kwenye hatua kama hii,, nimizuri, lakini tuseme hatuna bahati nayo na mashabiki wetu hawapaswi kukata tamaa kwani hayo ni mambo ya kawaida katika mchezo wa soka,”amesema Niyonzima.

Yanga imeondoka Zanzibar asubuhi, hii na inajiandaa na safari ya kuelekea Ruvuma ambapo Jumamosi itakuwa na mchezo wa ligi ya Vodacom dhidi ya Majimaji kwenye uwanja wa Majimaji Songea.

Advertisement