3131762

Nani Kuvunja Rekodi ya Mohamed Hussein (Mmachinga)


FEATURES

Yanga ina asilimia 95 ya kutetea taji lake msimu huu, hasa baada ya Azam kuambulia sare na JKT Ruvu na kupokwa pointi 3 baada ya kumchezesha Erasto Nyoni dhidi ya Mbeya City, aliyekuwa na kadi 3 za njano.

Achana na vita ya ubingwa, vita nyingine ipo kwenye ufungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara, Kiiza, Ngoma, Tabwe kila mmoja ana kitolea macho kiatu cha dhahabu.

Mohamed Hussein ndiye Mtanzania pekee anayeshikilia rekodi ya ufungaji wa magoli mengi Ligi Kuu Bara Mmachinga alifanikiwa kufunga magoli 26 kwa msimu, takribani sasa ni miaka 17 rekodi imendelea kudumu licha ya kujitokeza washambuliaji kadhaa ila hawakufanikiwa.

Article continues below

Abdallah Juma, mchezaji wa zamani wa Mtibwa alikaribia kuifikia rekodi ya Mmachinga kipindi alipotimiza magoli 25 mwaka 2006, na hakuweza kufikia rekodi hiyo hali kadhalika John Bocco, Bony Ambani na Kipre Tchetche.

Goal.com  inakuletea makala ya wachezaji ambao wanaweza kufikia au kuivunja rekodi ya Mohamed Hussein Mmachinga iwapo wataendelea kucheza katika kiwango walicho nacho au zaidi katika mechi zilizosalia.

Amis Tambwe

Kwa misimu 3 sasa amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, tayari ana magoli 20 msimu huu, bado magoli 6 kuifikia rekodi ya Mmachinga katika mechi 3 zilizo bakia, anaitaji wastani wa goli 2 au zaidi kwa kila mechi hili aweze fikia rekodi hii.

Hamis Kiiza

Mganda huyu tayari ametikisa nyavu mara 19 msimu huu, amebakiza mechi 4 msimu, hayuko mbali na rekodi ya Mmachinga hali kadhalika, anaitaji wastani wa goli 2 kila mechi.

Donald Ngoma

Hakuna amabaye ana mashaka na uwezo wa Donald ngoma, msimu wake wa kwanza ana magoli 16, yuko mbali sana kuweza kufikia idadi ya magoli 26 kwa mechi 3 zilizo bakia, wastani wa magoli 4 kwa mechi mmoja ni ngumu sana ingawa lolote linawezekana katika soka.

Advertisement