1vl26fmji9by71hxltz2dhxibq

Simon Msuva kujiunga na Manchester United

Kocha wa Manchester United, Jose Mourihno yuko mbioni kumnasa winga wa klabu ya Yanga na timu ya taifa Tanzania, Simon Happygod Msuva

Akizungumza  na vyombo vya habari leo tarehe 1 Aprili Jose Mourihno amethibitisha kuvutiwa na winga huyo wa Yanga  mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu na kila kitu kipo  kwenye hatua zamwisho ili kuipata saini ya nyota huyo

"Ni kweli tumekuwa tukimfuatilia Simon Msuva kwa muda mrefu sasa, mawakala wetu wapo Tanzania karibu mwezi ili kumalizana na klabu ya Yanga kuhusu dili hilo. Natumaini leo tarehe moja Aprili Msuva atakuwa ni mali halali kwetu.

"Kikubwa kasi yake uwanjani, uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi na pia kufunga ndiyo sababu kubwa kwetu kumsainisha Msuva, natumaini ataongeza ubora kwenye timu yetu hasa kwenye eneo la ushambuliaji ambalo lina upungufu mkubwa tangu aondoke Memphis Depay, alisema kocha huyo wa Man United, Mreno Jose Mourihno.

"Tarehe kama ya leo ni nzuri sana kwangu kwani ni siku ambayo naweza sajili mchezaji yoyote yule duniani nimtakaye", alimalizia Mourinho

Msuva anakuwa mchezaji wa nne kutoka Tanzania kucheza soka la kulipwa barani ulaya, baada ya Mbwana Samatta kukipiga Genk ya Ubelgiji, Farid Mussa Teneriffe ya Uhispania, na Ulimwengu aliyopo Swedeni

Msuva anaondoka Yanga akiwa mfungaji bora wa klabu yake kwa kufumania nyavu mara 20 kwenye mashindano yote, amefunga magoli 12 Ligi Kuu Bara, manne Mapinduzi, mawili klabu bingwa na mawili kwenye kombe la shirikisho TFF

Simon Msuva anatarajiwa kuondoka leo tarehe moja Aprili kuelekea Uingereza kwa ajili na kujiunga na Manchester United rasmi.

Watanzania kwa ujumla wako nyuma yake kwa ajili ya kumtakia mafanikio mema kwenye safari yake ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Nakutakiaeni Aprili Mosi njema :D

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0