1m1t628ks0dr21x9a9obgh7qm2

Nyota 11 wanaounda kikosi bora cha Barcelona cha muda wote

1xqimtmrdv6yh1xkt4mo5gjvyj

#1Victor Valdes | 2002-2014

Ndiye mlinda mlango aliyefanikiwa sana katika historia ya klabu ya Barcelona, mlinda mlango huyo ni mmoja wa nyota waliounda kikosi cha Catalunya kilichobeba mataji mengi katika kipindi chake

1nx2uq1y230e01971pa60169ab

#2Dani Alves | 2008-2016

Alijiunga na Barcelona akitokea klabu ya Sevila kwa dau la paundi milioni 30, tangu ajiunga hapo amekuwa mmoja ya mabeki bora Nou Camp na dunia nzima, alikuwa na msaada mkubwa kwa kutoa mchango mkubwa kwenye magoli kadhalika na ulinzi

56uvvjjlofzw1x2c4j8mkdwnb

#3Ronald Koeman | 1989-1995

Ndiye beki mwenye magoli mengi ndani ya Barcelona, amefanikiwa kufunga magoli 102 katika kipindi chake cha miaka 6 alichodumu na Wacatalunya hao. Koeman ana kumbukwa kwa kufunga goli la ushindi katika fainali ya Europe dhidi ya Sampdoria

1nswgamias4201hdem334knurt

#4Carles Puyol | 1999-2014

Ni mmoja wa wachezaji waliofanikiwa katika klabu ya Barcelona, mataji sita ya La liga na matatu ya klabu bingwa, Puyol ana sifika kwa roho yake ngumu ya kupambana na kupigania timu yake kwa muda wote alioitumikia Barca

12mdnk31jgqyqzpwg3za6d18z

#5Joan Segarra | 1949-1965

Kapteni wa Barcelona kwa miaka ya 1950, ni mchezaji wa tano ndani ya Barcelona alicheza mechi nyingi, Segarra alijitoa sana katika kuitumikia klabu hiyo katika kipindi chake

cp40sn1pxn181oo7ian8nn821

#6Johan Neeskens | 1974-79

Kiungo mwenye nguvu na mabavu, alikuwa anaweza kufanya kazi za nguvu kwa dakika 90 bila kuchoka

f795fw2lsshw1ixryvglj52l9

#7Xavi | 1998-2015

Mmoja wa viungo bora kuwahi kutokea Barcelona na duniani nzima, zao hilo la La masia limeche zaidi ya mechi 700 na kufanikiwa kunyakuwa mataji 25, kiungo huyo alikuwa ndiye moyo wa mfumo wa Tik Taka

xyhh6s9q42911py9lztseagho

#8Johan Cruyff | 1973-1978

Ndiyo nembo ya klabu ya Barcelona mafanikio yote wanayo jivunia Wacatalunya hao asilimia kubwa yamechangiwa na Cruyyff, mshindi huyo wa Ballon d'Or 3 amefanikiwa Barcelona kama mchezaji na kocha pia

tvjzvnx5o7vt1d036s7lq0ijh

#9Ronaldinho | 2003-2008

Mmoja wa wachezaji waliobalikiwa kipaji kikubwa cha kuuchezea mpira vile atakavyo, nyota huyo amefanya makubwa ndani ya Catalunya na ni vigumu jina lake kufutika mapema kwa mashabiki wa soka hasa wale wa Barcelona

49jwqvevxgm51pp5j047vx2o3

#10Andres Iniesta | 2002-

Kiungo bora mchezeshaji katika historia ya Barcelona, amekuwa sehemu muhimu ya kikosi tangu enzi za Pep Guardiola hadi sasa

6e8skn2vg5lz1pea1kqhblna4

#11Lionel Messi 2004-

Inasemekana ndiye nyota bora kuliko wote walio wahi pita Barcelona, mshindi huyo wa tuzo tano za Ballon d'Or ndiye mfungaji bora wa muda wote katika historia ya klabu hiyo

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0