Baada ya Ligi Kuu kumalizika majuma mawili yaliyopita kwa kushuhudia klabu ya Yanga wakifanikiwa kutetea taji lao la Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo, sasa ni kipindi cha usajili, kila klabu inajaribu kuimarisha timu yake kwa kusajili nyota ambao watakuja kuimarisha kikosi kwa msimu ujao
Majina mengi ya wachezaji yamekuwa yakihusishwa kwenda klabu mbali mbali kwa kipindi hiki cha usajili, klabu mpya ya Singida United imekuwa gumzo kipindi hiki cha usajili kwa matumizi makubwa wanayotumia na kuzipiga vikumbo timu kubwa za Simba, Azam na Yanga
Goal inakuletea wachezaji wanaowindwa sana dirisha hili la usajili
Ibrahim Ajib
Ameshamalizana na klabu yake ya Simba, Ajibu ni mchezaji huru kwa sasa, mshambuliaji huyu ni lulu kipindi hiki kwani kila kukicha amekuwa akitolewa macho na klabu za Azam, Yanga na Singida
Kuna dalili kubwa nyota huyo ya kujiunga na klabu ya Singida United kwa mkataba wa miaka miwili
Ibrahim Ajibu maongezini na Singida United
Donald Ngoma
Bado ajasaini mkataba mpya na klabu yake ya Yanga, Ngoma amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu Simba kwa ajili ya Msimu ujao, matajiri wa Msimbazi wako tayari kuvunja benki ili kupata Huduma ya Mzimbabwe huyo
Jonas Mkude
Kama ilivyo kwa nyota wengine, Mkude naye amemaliza mkataba na Simba hivyo ni mchezaji huru, Mkude anatazamiwa kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu klabu ya Yanga, usajili wake umekuwa ukitajwa tangu msimu ujamalizika
Aishi Manula
Klabu za Simba na Singida United zinapigana vikumbo kwa ajili ya kuipata saini ya mlinda mlango huyo bora wa Msimu huu, Manula na Azam bado wapo kimya kwenye suala la kuongeza mkataba hivyo kuzidi vipa nguvu klabu zingine kumnyemelea
Youthe Rostand
Mlinda mlango wa klabu ya African Lyon, Mcameroon huyo licha ya klabu yake kushuka daraja ila ni mmoja wa magolikipa waliyofanya vizuri msimu uliopita, Simba na Yanga zimekuwa ziki ulizia Huduma ya mlinda mlango huyo
Raphael Daud
Baada ya kuondoka Kenny Ally Mbeya City, kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ya Mbeya kumpoteza tena winga wao bora Raphael Daud, klabu za Yanga na Azam ziko tayari mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu
