+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
1t5gwbyl01dbf14rvgpm0r2umd

Simba wakamilisha usajili wa John Bocco

Mshambuliaji John Raphael Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba, baada ya kumalizana na timu aliyoichezea kwa misimu 10 mfululizo Azam FC.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, ameiambia Goal, wameshamalizia na Bocco, na kwasasa ni mali yao hivyo msimu ujao ataonekana akiwa amevalia jezi nyekundu na nyeupe.

“Nikweli Bocco tumemalizana naye baada ya kumpa mkataba wa miaka miwili ni mchezaji mzuri ambaye hata kocha Joseph Omog ameridhishwa na usajili wake,” amesema Hans Poppe.

Bocco alitaka dau la Sh. Milioni 40 kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kucheza Azam FC kwa mshahara ule ule wa Sh. Milioni 4, lakini uongozi chini ya Meneja, Abdul Mohammed haukukubaliana naye.

Azam ilikuwa tayari kuendelea kumlipa Sh. Milioni 4 Bocco, lakini katika upande wa dau la usajili alitakiwa kuchukua Sh. Milioni 10 na mchezaji huyo akakataa.  

Kwa kuwa Simba imefanikiwa kurejea kwenye michuano ya Afrika mwakani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 na ipo kwenye harakati za kuboresha kikosi, ikaona ni vyema kutoa Sh. Milioni 40 kumsajili mfungaji huyo bora wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Na baada ya kusaini mkataba huo, Bocco ambaye ataendelea kulipwa Sh. Milioni 4, ameingia kwenye mazoezi makali ya kujiweka fiti zaidi ili akaweze kukabiliana na changamoto ya ushindani wa namba dhidi ya washambuliaji hatari wa Simba, Laudit Mavugo na Juma Luizio.

Bocco alijiunga na Azam FC mwaka 2007 akitokea Cosmopolitan ya Dar es Salaam na akaisaidia Azam FC, kupanda Ligi Kuu mwaka 2008 akiibuka mfungaji bora wa Daraja la Kwanza.

Baada ya hapo, Bocco akawa mshambuliaji tegemeo wa Azam FC akiiongoza kutwaa mataji kadhaa, ikiwemo Ligi Kuu mwaka 2014 na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, au Kombe la Kagame mwaka 2015.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0