+18 | Commercial Content | T&C's Apply | Play Responsibly | Publishing Principles
2715602

Kikosi Bora cha Muda wote Yanga

1.Joseph Fungo
Kipa mwenye mafanikio makubwa ambaye hajapata kutokea hadi leo mwanzoni mwa miaka ya 1980, aliweza kuidakia timu hiyo misimu miwili peke yake na kuipa ubingwa mwaka 1981 na mwaka uliofuata Yanga ilikutana na Simba ambayo ilitoka kuweka Kambi nchini Brazili licha ya Simba kushambulia kwa muda wote wa mchezo lakini kipa huyo alikuwa kikwazo kwa kudaka mipira yote ya hatari na matokeo kuwa sare ya 0-0.

2.Yusuf Bana
Beki bora aliyepata kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa katika kipindi chake alikuwa na uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira lakini pia alikuwa ni mtaalamu wa kurusha mipira kwa umbali mrefu zaidi ya Mbuyu Twite.

3.Kenneth Mkapa
Beki huyu wa kushoto alikuwa na mafanikio makubwa kwenye timu ya Yanga, sifa yake kubwa ilikuwa ni kucheza nafasi zaidi ya moja na hiyo ilitokana na uwezo wake wa kutumia miguu yote miwili pamoja na mara nyingi kutumiwa kama beki lakini ilikuwa ni mara chache sana kumuona akicheza rafu na Yanga ilikuwa ikimtegemea kuanzisha mashabulizi.

4.Athuman Juma Chama
Chama alipata sifa kubwa sana wakati akiichezea Yanga na hiyo ilitokana na kutimiza ipasavyo majukumu yake ya kuwadhibiti washambuliaji hatari wa timu pinzani mara zote walipo kutana na wapinzani wao Simba kipindi hicho aliweza kumdhibiti vizuri Zamoyoni Mogela na kushindwa kuonekana licha ya ukali aliokuwa nao.

5.Godwin Aswile
Beki wa kati aliyepata sifa kubwa kutokana na uchezaji wake wa kutumia nguvu na akili kwa pamoja huku akiziba vizuri makosa ya mabeki wake wapembeni pindi inapotokea wamepitwa katika kipindi chake cha uchezaji aliweza kuisaidia Yanga ubingwa wa Tanzania mwaka 1993.

6.Issa Athuman
Kiungo mkabaji aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kuwadhibiti viungo wa timu pinzani Athuman, alijizolea sifa kuwa akiwa na Yanga kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kucheza vizuri nafasi za nyuma na hata kiungo mchezeshaji kwa sasa ni marehemu.

7.Akida Makunda
Winga hatari wa pembeni ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kuipa Yanga ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1997 kule nchini Uganda, tangu aondoke yeye Yanga bado haija mpata mchezaji wa aina yake ingawa wamepita akina Mrisha Ngasa na Said Maulidi.

8.Athuman China
Ukiwatoa Haruna Niyonzima na Selvator Edward Yanga bado haijaweza kupata kiungo mwenye uwezo wa kuuchezea mpira kama ilivyokuwa kwa Chama, mchezaji huyo ambaye alisifika kutokana na uwezo aliokuwa nao na kupewa jina la mapafu ya mbwa kutokana na muda wote wa dakika 90, kupambana kuipigania timu yake.

9.Abeid Mziba
Mshambuliaji huyo aliyefanya vizuri kipindi chake cha uchezaji sifa yake kubwa ikiwa ni ufungaji wa mabao kwa kutumia kichwa ingawa kwa sasa yupo Amissi Tambwe, lakini Mrundi huyo bado hajafikia uwezo aliokuwa nao Mziba ambaye kipindi chake hakuwa na mpinzani katika mabao ya vichwa.

10.Said Mwamba
Huyu ni kiungo mshambuliaji aliyepata umaarufu mkubwa akiwa na kikosi cha Yanga, sifa zake hazipishani sana na zile za Keneth Mkapa kutokana na uwezo wa kucheza nafasi tofauti , katika ligi ya mwaka 1999 aliweza kuibuka mfungaji bora ingawa kocha wake wa wakati huo Tambweleya alikuwa akimtumia sana kwenye nafasi za ulinzi.

11.Edibily Lunyamila
Mmoja ya mawinga hodari walio wahi kutokea Tanzania katika kipindi chake cha uchezaji Yanga ilifanikiwa kukizi haja za mashabiki wake kutokana na uwezo aliokuwa nao mchezaji huyo ambaye pia alisifika kwa mataifa ya jirani Afrika Mashariki na Kati kwa jina lake kuandikwa kwenye magari mchango wake kwa Yanga aliweza kuipa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1997.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0