+18 | Play Responsibly | T&C's Apply | Commercial Content | Publishing Principles
sqo6bev15w6c1475z410ew5rh

Al Jadida yatangaza usajili wa Simon Msuva kutoka Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva ametambulishwa rasmi na klabu yake mpya Difaa Al Jadida ya Morocco baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo.

Al Jadida imepandisha picha kibao katika ukurasa wake wa Facebook zikimuonyesha Msuva akiwa na Tiboroha kuanzia anasaini, anakabidhiwa jezi hadi anatambulishwa kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.

Hata hivyo, si Msuva wala Difaa aliyesema ni mkataba wa miaka mingapi, mchezaji atakuwa analipwa kiasi gani na klabu yake wala Yanga imepata kiasi gani.  

Ingawa mapema tu habari zisizo za uhakika, zilisema Difaa ambayo tayari imekwishamchukua Mtanzania mwingine, winga pia Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Azam FC ya Dar es Salaam pia, itailipa Yanga dola za Kimarekani 150,000 tu kwa kuwa Msuva alikuwa amebakiza miezi tisa katika mkataba wake.

Msuva alijiunga na Yanga SC mwaka 2012 akitokea Moro United iliyokuwa tayari imehamishia maskani yake Dar es Salaam kutoka Morogoro na awali ya hapo alipitia akademi ya Azam baada ya kuibuliwa na iliyokuwa taasisi ya Pangollin ya kocha Charles Boniface Mkwasa, ambaye sasa ni Katibu wa Yanga, klabu aliyoichezea na kuifundisha awali. 

Baada ya kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mfungaji bora mara mbili – bila shaka sasa ni wakati mwafaka kwa Msuva kwenda kutafuta changamoto mpya nje ya nchi. 

Timu hiyo yenye maskani yake mji wa Al Jadida ikiwa inatumia Uwanja wa El Abdi inataka kuwatumia mawinga wa Tanzania kujaribu kutwaa taji la kwanza la Ligi Kuu ya Morocco, inayojulikana kama Botola, moja ya Ligi bora kabisa barani Afrika.

Advertisement

ENJOYED THIS STORY?

Add GOAL.com as a preferred source on Google to see more of our reporting

0