Lionel Messi akana kumtusi mwamuzi, Alitukana hewani si mwamuzi

Comments
Lionel Messi matusi aliyotoa hayakumlenga mwamuzi, aliyasema tu hewani hivyo adbabu hiyo ifutwe isiwe juu yake

Nahodha wa Argentina Lionel Messi amekana madai kuwa kwa kinywa chake alimtusi mwamuzi msaidizi nchi yake iliposhinda 1-0 dhidi ya Chile wiki iliyopita.

Messi, 29, alifungiwa mechi nne za kimataifa masaa machache kabla ya mechi ya Jumanne kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia, baada ya kumwelekezea "maneno ya matusi" mwamuzi msaidizi katika mechi ya wiki iliyopita.

Wengi wameshangaa jinsi Messi alivyopewa adhabu hiyo na Barcelona nao walitoa tamko leo kuponda adhabu hiyo ya kufungiwa mechi nne.

Alhamisi, Lionel Messi alitoa taarifa isomekayo: "Nakanusha vikali kumshambulia mwamuzi msaidizi kwenye mchezo dhidi ya Chile, kwa maana hiyo siamini kama nimevunja nidhamu ya FIFA kufungu namba 57.

"Mwamuzi msaidizi, mwenye uraia wa Brazili, alielewa vema kile nilichokuwa nasema, sana tu na tuliongea vema na sikutumia lugha mbaya dhidi ya refa huyo.

Article continues below

"Ikiwa lolote katika maneno yangu halikumpendeza mwamuzi msaidizi, hayakuelekezwa kwake lakini hewani, si kwake, naomba radhi. Hivyo basi naomba shauri hili la kinidhamu lifutwe bila adhabu juu yangu."

Adhabu ya kufungiwa mechi nne ni kwenye mechi za Argentina tu, Messi ataendelea kukosa mechi za Uruguay, Peru, Venezuela na Ecuador.

 

Next article:
Arsenal should be making Ramsey captain, not letting him leave - Wilshere
Next article:
'Slavery was abolished a long time ago' - Hazard will leave Chelsea, says ex-Real Madrid president
Next article:
ISL 2018-19: Mumbai City FC vs FC Pune City - TV channel, stream, kick-off time & match preview
Next article:
Sarachan's stint as the friend-zoned USMNT coach winding to a close
Next article:
ISL 2018-19: Delhi Dynamos pay the price for wayward finishing
Close