Victor Wanyama atua Tanzania kwa mapumziko

ShirikiFunga Maoni
Mchezaji wa kimataifa wa Kenya anayekipiga Tottenham, Victor Wanyama ametua Tanzania kwa mapumziko ya wiki mbili akisubiri Ligi Kuu Uingereza kuanza

Kiungo wa kimataifa wa Kenya na klabu ya Tottenham Hotspurs, Victor Wanyama amewasili Tanzania leo asubuhi kwa ajili ya mapumziko mafupi kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Uingereza.

Mchezaji huyo aliyefanya vizuri kwenye msimu wake wa kwanza chini ya kocha Mauricio Pochettino, ameiambia Goal, amechagua Tanzania kwa ajili ya mapumziko kwa sababu ni sehemu tulivu tofauti na Kenya.

“Nimekuja Tanzania kwa sababu ni sehemu tulivu ambayo itanisaidia kutuliza akili yangu kujiandaa na msimu ujao lakini pia kuna sehemu nzuri za kuvutia hapa naamini kwa muda nitakaokaa hapa wa wiki mbili nitafurahia mapumziko yangu,” amesema Wanyama.

Wanyama Victor akiwasili Tanzania

Kiungo huyo amesema siyo mgeni wa Tanzania kwa sababu amewahi kuja mara kadhaa akiwa na timu yake ya Taifa ‘Harambee Stars', lakini ujio wake wa safari hii ni tofauti kwa sababu amekuja kwa mapumziko na siyo kikazi.

Wanyama pia amezungumzia maandalizi yake kwa ajili ya msimu ujao na kusema amejipanga kuweza kuisaidia zaidi timu yake ili kutwaa ubingwa wa ligi ya Uingereza baada ya msimu uliopita kumaliza nafasi ya pili.

Amesema kwake ilikuwa ni mafanikio makubwa kumaliza nafasi ya pili, pamoja na mchango mkubwa alioutoa kwa timu yake hata kocha wake Pochettino kumwamini na kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Makala Inayofuata:
Bado mapema sana kuzungumzia ubingwa 'Lwandamina'
Makala Inayofuata:
Tunalazimika kupambana ili kutimiza malengo 'Okwi'
Makala Inayofuata:
Aristica Cioaba 'Nitawafunga Mbao mbele ya mashabiki wao'
Makala Inayofuata:
Pep Guardiola ahofia kumpoteza Kevin De Bruyne
Makala Inayofuata:
Edinson Cavani anataka kwenda Manchester City
Funga