Mabao ya Chirwa yawapoteza Ajibu na Nyoni wa Simba

ShirikiFunga Maoni
Baada ya kufanya kazi kubwa hatimaye Obrey Chirwa wa Yanga, ametangazwa mchezaji bora wa ligi ya Vpl, wa Oktoba, kutokana na mabao yake

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga raia wa Zambia,  Obrey Chirwa,  amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Oktoba, kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa timu yake ambayo anaitumikia kwa msimu wa pili sasa tangu asajiliwe akitokea FC Platinum ya Zimbabwe.

Msemaji wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Alfred Lucas ameiambia Goal, Chirwa ameibuka mshindi kwa kuwapiku wapinzani wake wa karibu mshambuliaji mwenzake wa Yanga Ibrahim Ajibu na beki wa Simba Erasto Nyoni, ambao nao walijikuishwa kwenye kinyanganyiro hicho.

Lucas amesema katika mwezi huo Yanga iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba,  ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja, pia Yanga iliifunga Stand United mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.

Kiwango cha mchezaji huyo kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao la Yanga lilifungwa na Chirwa, hivyo kwa mwezi huo alifanikiwa kuwa na kiwango cha juu katika kila mchezo ikiwa ni pamoja na kufunga.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba).

Makala Inayofuata:
Timu ya wiki Ligi Kuu Uingereza: De Bruyne na Salah waongoza
Makala Inayofuata:
Barcelona yataja mbadala wa Gerard Pique
Makala Inayofuata:
Real Madrid imetenga £53m kwa ajili ya Sergio Aguero wa Manchester City
Makala Inayofuata:
Yanga Yaifukuza Simba kimya kimya
Makala Inayofuata:
'Nataka kubaki Tottenham miaka yote' - Kane afunika tetesi za Brazili
Funga